VISAKRAMENTI
Visakramenti ni Baraka za kanisa juu ya watu au vitu na mahali. Lengo la visakramenti ni kuwaandaa watu kupokea tunda la sakramenti na kutakatifuzwa mazingira mbalimbali ya maisha tunamoishi. Tunatumia visakramenti kwa sababu vinatusaidia moyoni na mwilini na vinatuongezea imani na kuleta msaada wa Mungu. Tunapaswa kutumia visakramenti kwa imani kwa matumaini ya kupata ulinzi wa Mungu kwa ajili ya Baraka ya kanisa. Visakramenti vinatusaidia kuongeza moyo wa imani na uchaji, hutusaidia kujipatia neema mbalimbali pia kujipatia misaada ya mwili na roho na zaidi sana hutusaidia kukingwa na maovu na kutakaswa na maovu. 
Tunapotumia visakramenti inapaswa tusivichukulie nafasi ya Mungu wala tusijitie hatarini bila sababu kwa kutmia kama ulinzi wetu. Visakramenti vitumike kwa ibada, visakramenti vinavyotumika mara nyingi ni Rozari, misalaba, medali, skapulari, maji ya Baraka, chumvi, mishumaa n.k. 

SKAPULARI YA KAHAWIA
Bikira Maria alimtokea Mtakatifu Simon Stock katika mlima Karmeli mwaka 1251, alimkabidhi skapulari ya kahawia. Aliahidi kwa kusema maneno yafuatayo “Yeyote atakayekufa amevaa skapulari hii hataingia katika moto wa jehanamu”. 

Ahadi nyingine za skapulari ya kahawia ni:-

  1. Alama ya wokovu
  2. Kinga dhidi ya hatari 
  3. Amana ya amani 

Kwa nini tunavaa skapulari?

  1. Majitoleao ya Mama Bikira Maria
  2. Kujipatia Rehema na Neema 
  3. Utii kwa Ombi la Mama Bikira Maria 
  4. Skapulari ni vazi la Mama Bikira Maria lililotengenezwa kwa sufi na ni lazima livaliwe juu ya mabega katika mtindo ambao upande mmoja unaning’inia mbele ya mwili na upande mwingine unaning’inia mgongoni. 

FADHILA YA JUMAMOSI
Fadhila ya jumamosi inahusika na ahadi ya Bibi yetu ya kuwaondoa watu katika mateso ya toharani jumamosi ya kwanza baada ya kufa kwao wale ambao walitimiza masharti yafuatayo;-
Kuvaa skapulari kwa uaminifu 
Kutunza usafi wa moyo kadri ya maisha yao 
Kusali kila siku ofisi ndogo ya Mama yetu mbarikiwa; kwa wale ambao wako kwenye Rozari Hai, Ruhusa maalum imetolewa kwamba makumi yao wanayosali kila siku yaweza kuwa badala ya Ofisi ndogo. 

MATUMIZI YA SKAPULARI YA KAHAWIA
Ibarkiwe na padre
Ivalishwe na padre (ikiwezekana)
Ivaliwe shingoni
Ikichakaa istupwe hovyo
Katika matumizi ya skapulari ya kahawia kumekuwepo na matukio mbalimbali ya miujiza ambayo imethibitishwa na kanisa. Miujiza hiyo ni pamoja na nyumba iliyonusurika kuungua moto, ajali ya treni, padre aliyenusurika kwa kupigwa risasi, kijana aliyenusurika kuungua katika mlipuko wa petrol, watu waliobadilishwa maisha na kuwa katika maisha ya uchaji, walionusurika katika ajali ya baharini, watu wawili walionusurika vitani na miujiza mingine  mingi ambayo haikuandikwa popote. 
Kwneye uvaaji wa skapulari anachokifanya Mama Bikira Maria ni kumbadilsha mtu kwa maombezi yake kwa Mungu. Akae katika mwelekeo wa kumjua Mungu na ndiyo maana ya hiyo miujiza ili mtu aamini na marudie Mungu na kweli kuna waliomrudia Mungu kwa njia hiyo ya miujiza ya Skapulari ya kahawia. 
Kuvaa skapulari ya kahawia ni kama uko kwenye sala, mama bikira maria alisema “unapovaa skapulari ni kama unanifikiria mimi name nitakuwa nakufikiria”. 
Mwaka 1920 Mama Bikira Maria alimwambia mmoja wa wale watoto wa Fatima kuwa zitakuja fasheni za nguo ambazo zitamchukiza sana mwenyezi Mungu mnaomtumainia Mungu msifuate hayo; badala yake vaeni skapulari. 

MAMBO MUHIMU
Tusivae tu skapulari bila kuamua kutenda mema, pia skapulari itumike kwa ibada
Tukitumia skapulari vizuri itatuelkeza kwenye utakatifu aidha kwa kuvaa skapulari mazuri yaliyo ndani yetu yanakuzwa. 
Inasemekana kuwa katika kanisa katoliki hakuna skapulari iliyothibitishwa kuwa na miujiza mingi kama skapulari ya kahawia.
Katika kanisa katoliki zimethibitishwa skapulari 18 ikiwemo skapulari ya kahawia.
Skapulari ya kahawia inaweza ikawa na picha au isiwe na picha pia inaweza iwe na maandishi au isiwe nayo
Skaplari inapochakaa kwa kuwa ni kitu kitakatifu, haipaswi kutupwa katika majalala ya takataka bali inapaswa aidha izikwe au ichomwe. 
Kila wakati unapobusu skapulari ya kahawia kwa ibada ukiwa katika hali ya neema ya utakaso unapata rehema ya siku 500.

Mtu akivalishwa skapulari ya kahawia na Padre kwa ibada atapata chapa ya maisha ya skapulari kwa maana kwamba akipata skapulari nyingine hana haja ya kuibariki ataivaa tu kwa kuwa Baraka za mwanzo zitaambatana naye.