MTAKATIFU FILOMENA 
MWANGA MPYA KATIKA GIZA

AMANI KWA FILOMENA
Baada ya miaka 1500 ya kusahaulika kwenye makaburi, tarehe 24.5.1802, Sikukuu ya Bikira Maria Msaada wa wakristo wachimbuwaji waliokuwa wakiondoa mawe na mchanga (vifusi) katika makaburi ya zamani yaliyofahamika kwa jina maarufu Priscillas Ground na kubomoa sehemu zilizo kuwa zimesakafiwa walisimamisha kazi hiyo walipogundua kaburi lililokuwa pembezoni. Walipochunguza Zaidi walishangazwa kuona kaburi lililokuwa katika hali nzuri na imara, lenye kuta tatu na kupambwa kwa vigae marumaru waliozikwa kwa jinsi hii walikuwa watu maarufu sana au mashahidi waliwekwa kwenye jeneza la marumaru nakufunikwa vizuri. Baada ya kugundua haya walimpa taarifa mlinzi wa makaburi hayo na aliamuru kazi ya uchimbuaji isimamishwe. Jiwe la maziko lilitofautishwa kwa alama za mitende na yungiyungi, mishale na nanga ziliashiria kuwa aliyezikwa hapo ni shahidi. Ambaye ni Mtakatifu Filomena aliyekuwa bikira aliyechomwa kwa mishale na alifungiwa kwenye nanga. Maneno yaliyo kutwa juu ya kaburi lake yalipopangwa vizuri yalisomeka “PAX TECUM FILUMENA” au “PEACE TO YOU FILUMENA” yaani “Amani kwako Filomena.”

Kaburi lilipofunuliwa ilipatikana mifupa midogo na fuvu lililovunjika la msichana mdogo. Wachunguzi walibaini kuwa alikuwa msichana wa miaka 12 au 13 alipouwawa. Chombo kidogo kilichovunjika kilikutwa ndani ya kaburi kilikuwa na kitu kilichokauka rangi nyeusi, nyekundu au hudhurungi. Wanasayansi walithibitisha kuwa ilikuwa ni damu iliyokauka. Nyakati hizo wakristo walikusanya damu za mashahidi na kuziweka pamoja na miili yao kaburini. Wataalamu walipoendelea na uchunguzi wa kilichokuwa kwenye chombo kile walishangazwa na majibu ya ajabu, ya kikemikali chembembe ndogo zilipochukuliwa na kuwekwa kwenye chombo safi, kulitokeza vituo vilivyo ng’ara sana, vituo hivyo vilionekana vya thamani sana kama vile dhahabu na madini ya fedha. Wanasanyansi na watazamaji wengine waliliangalia kwa heshima kubwa tukio hilo la kitakatifu.

Ukweli kwamba mabaki ya mwili wa Mtakatifu Filomena yalikutwa kwenye makaburi ya zamani yaliyofahamika kama “Priscilla’s Ground” hivi yathibitisha kuwa alikuwa mtu wa heshima kwani “Priscilla’s Ground” lilikuwa maarufu kwa picha za Sanaa zilizokuwa zimechorwa humo na zilikuwa nzuri sana. Katika ukuta wa makaburi haya pia aliwakilishwa (alichorwa) mwanamke bikira na mtoto, ambavyo kumbukumbu zake zinaonyesha karne ya pili, pia kuna mchoro wa picha ya karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake. Penye makaburi haya yalipatikana pia mabaki basilica dogo lililojengwa na baba Mt. Silivesta na ndimo alimozikwa yeye na mapapa wengine wane.

Miaka mitatu baadae, Augusti 10, 1805 mabaki (masalia) ya Mt. Filomena yalitolewa kutoka Naples kupelekwa mahali pa heshima huko Mugnano, Italia. Mabaki hayo yalipofikishwa karibu na nyumba yalipokuwa yahifadhiwe kwa muda huko Mugnano, kimbunga kilizuka na kuwahofisha watu waliokuwa wakisubiri usafiri wa gari, kimbunga kile kilipokaribia masalia ya Mt. Filomena kiliacha kuvuma. Padre aliyekuwa ameyabeba alisema kwa sauti ya ari kubwa, wakristo, msiogope, hizi ni salamu kutoka kwa binti Mfalme wa giza anayefahamika sana kama shahidi Mtakatifu wa ushindi wake wa juu ya utawala wote wa giza. Sasa shahidi huyu anayefahamishwa kwa watu kama nyota ing’aayo, itokayo katika giza la maziko kwa mastahidi yake macho ya Mungu yashuhudia ushindi wa roho mbinguni na kushinda vita dhidi ya wasioamini na roho chafu, zilizohukumiwa. Kwa maombezi yake tunapata neema nyingi ambazo Mungu amemjalia. Ndiyo maana maadui wabaya wa huyu Mtakatifu wanaonyesha ishara ya kuumizwa, kuaibishwa na kukukatishwa tamaa.
Miaka 35 baada ya kugunduliwa kwa masalia hayo, huyo Binti mdogo wa kifalme Mgiriki, alitangazwa kuwa  ni mtakatifu na mtenda miujiza wa karne ya 19.Papa Gregori XVI, mnamo tarehe 30 Januari, 1837 alimtangaza kuwa ni Mtakatifu akaidhinisha ibada yake katika ulimwengu kwa wakatoliki milele yote….Wakati Mawakili wa Rozari Hai walipojinyenyekesha miguuni mwa Papa, Mkuu wa kanisa, aliridhia kutoa Baraka maalumu kwa umoja huu chuni ya usimamizi wa Mt. Filomena akitamka maneno haya: Tangu leo Rozari Hai iko chini ya Ulinzi wa Mt. Filomena!
Mt. Filomena alitenda maajabu mengi na miujiza kwa maombezi yake yenye nguvu kwa Mungu.

“KWA FILOMENA HAKUNA OMBI LINALOKATALIWA!”
SALA KWA MT. FILOMENA.
Ee Mtakatifu Filomena, Bikira Shahidi, ambaye Mungu amekutukuza kwa wingi wa miujiza na ambaye halifa wa Yesu Kristo amekuita “mlinzi wa Rozari hai na wa watoto wa Maria” dhihilisha Zaidi na Zaidi kutoka vilele vya uwinguni kwa sauti takatifu kama yako haiwezi kukataliwa kitu na kwamba tuna haki ya kutegemea msaada wako. Tujalie neema ya kuwa waaminifu kwa Yesu hata ikitupasa kufa.  Amina.

Wakati watakatifu wengine wamepewa uwezo wa kutusaidia katka shida moja au nyingine, Mt. Filomena yeye amepewa uwezo wa kutusaidia katika kila shida; iwe ni mahitaji ya kiroho au ya kimwili. Hebu tumwendee kwa matumaini makubwa tukiiwa na imani na mapendo. Yeye ni “BINTI MPENDWA” wa Yesu na Maria ambaye kwake hakuna chochote kinachokataliwa.