Kila mwanachama wa ushirika wa Rozari Hai, anaombwa atoe chochote kwa ukarimu wake na kwa hiari yake mwenyewe, kwa lengo la kusaidia gharama za Utume huu. Mchango huu utatumika kununulia misalaba, medali, Tasbihi, Skapulari, picha za watakatifu, vijitabu vya ibada kwa kusaidia ibada ya wakristu n.k. Pia michango hii itasaidia kununua karatasi na kalamu za ofisini na kulipia gharama ya uchapishaji, kwa kusaidia utume huu uendelee vizuri. Kutoa ni moyo si Utajiri. Mwanachama anaweza kutoa chochote kile awezacho na/au kutolea sala na sadaka ndogo ndogo kwa kuleta ufanisi na ustawi wa ushirika huu wa Rozari Hai. Rozari Hai ni familia yako. Familia hii inaweza kufanya kazi, kukua, kueneza ujumbe wake na kubadili Dunia kadiri wewe unavyochangia kutoa chochote. Kwa njia ya mchango wako Ushirika huu utapata kukua na kuwa na nguvu sana. KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI!