“MTU MASHUHURI KWA KANISA ULIMWENGUNI, MWANZILISHI
WA KAZI ZA KIMISIONARI DUNIANI.”
Mwenyeheri Paulina Maria Jaricot alizaliwa tarehe 22 July 1799 na alifariki tarehe 9 January 1862 Lyon, Ufaransa. Huyu ndiye mwanzilishi wa Rozari hai Ulimwenguni. Alipata kwa haki kuwa msimamizi wa walio katika dhiki ya fedha. Yeye ni mama wa masikini, wakili wa wadaiwa, msaada kwa waliofanyiwa hila, walioteswa na kudhalilishwa “mwombe Paulina ambaye aliteseka sana, kutokana na wenye ubinafsi, uroho na majivuno. Atasikia sala zako, Kuufanya mzigo wako kuwa mwepesi na kukupatia Baraka za pekee unazohitaji katika kuubeba msalaba wako mzito kwa ujasiri na matumaini.”
Moyo wa Paulina ni mwepesi na ataponya majeraha yako kutokana na upako aliyoupata kwa Mungu kupitia mateso na mahangaiko aliyopitia kila uchao.
Paulina Maria Jaricot aliaminishwa na mwangalizi wake Mt. Jean Marie Vianney ambaye anasema: “Mara nyingi duara la mwanga lilionekana katika kichwa cha Mama yetu Paulina wakati akiwa katika sala zake za muda mrefu mbele ya Ekarist Takatifu.”
Kuna nyaraka nyingi zinazoeleza zawadi ya pekee ya unabii aliyokuwanao Paulina. Watunzaji wa nyaraka za Paulina Jaricot wametoa masalia ya damu, kipande cha nguo ambacho moyo wake ulilala na kuchanganywa kwenye damu ya huyu mwasisi wetu mpendwa.
SALA KWA MAOMBEZI Y A MWENYEHERI PAULINA MARIA JARICOT
EE PAULINA! Uliwahi kuwa tajiri, mzuri na kupendwa, tena ukawa masikini na mwenye taabu na uliyedharauliwa. Tusaidie sisi kubeba umasikini, taabu na dharau, upole, au kuzidi kiasi, kwa mapenzi ya Mungu, wokovu wa roho na kwa ulinzi wa Imani katika usafi wake wote. Wewe ulikuwa mtoto wa saba katika familia ya watu tisa, baba yako alikuwa mzaliwa wa kumi na tatu aliyezaliwa katika familia ya kimasikini lakini wakalimu. Tusaidie kukubali kujisalimisha kwa upendo, watoto wote Mungu anaotukabidhi kuwalea, na utupatie uwezo unaotakiwa kuwapatia mahitaji yao yote ya kiroho na kimwili.
EE PAULINA! Ulikuwa na matumaini makubwa kwamba jumuiya yako ya kikristo ingewapatia hali ya umoja ambapo familia zingekaa pamoja, kuongezeka kuwa na malezi yakina. Katika mwisho huu, utakuwa umewekeza rasilimali na kukopa sana, ukijiwekea Imani; Akiba ya Mbinguni.
KIKOMBE GANI CHA UCHUNGU ulichokuwa nacho, ulipogundua kuwa wale uliowaamini kwa mali zako za duniani walikuwa wezi wachukuwaji kilaini, ambao walikudanganya wewe kwa mali zako zote bila ya nafasi ya kupumua hadi kifo, ulijitahidi sana kuwalipa wadeni wako. Licha ya uchungu wa maumivu makali yaliyoletwa na ufukara wako, ulishambuliwa vibaya na wadaiwa wako na mahakama, ulipuuzwa, ulidharauliwa na ulikebehiwa na rafiki na adui pia.
EE PAULINA! Jinsi gani ulivyoweza kubeba kishujaa huu msalaba mzito kwa utukufu wa Mungu! Jinsi gani kwa upendo ulivyokubali fedheha zilizolundikwa juu yako! Kwa hekima ya milele uliyaweka mateso yako katika Moyo mororo wa Yesu kupita Moyo Safi wa Malkia wa Mashahidi.
TUNATAKA KUKUKPA HESHIMA, Mwenyeheri Paulina Marie Jaricot, kama mlezi wa wadeni kwa dunia nzima tuombee sisi na kwa wote wanaohitaji maombezi yako. Utupatie kwa ajili yetu uwezo wa kulipa madeni yetu kikamilifu au tuachiwe huru kutoka kwenye hayo lakini muhimu Zaidi, tusaidie, kubeba hilo kwa uvumilivu kwa utukufu wa Mungu.
EE MOYO WA PAULINA tanuru ya mapendo kwa binadamu wote, nifariji na nisaidie katika hitaji langu, (………hapa jata ombi lako) umempenda Yesu Kristo Zaidi kuliko yote, kwa ajili ya upendo wake, umewapenda wale walio katika taabu na mateso kuliko unavyojipenda mwenyewe..
Baba yetu……………….. Salamu Maria…………….. Atukuzwe Baba………..