Mkristu yeyote anayetaka anaweza kujiunga na ushirika huu wa Rozari Hai. Anaruhusiwa kujiunga mkristu wa umri wowote aliye tayari kusali kumi atakalopewa na makao makuu. Kitu cha muhimu ni kwamba mkristu awe tayari kusali kumi lake atakalopewa, kila siku kwa maisha yake yote. Moja ya faida kubwa ya Rozari hai ni kwamba: watu wema watendelea kuwa wema zaidi, na wakosefu watapata Neema ya kumgeukia Mungu na kuacha njia zao mbaya, ili nao wawe wema.
Kila siku mwanachama atajitahidi kusali lake na kutafakari fumbo linalohusika na kumi hilo, akiungana na wanachama wenzake, hasa wale wa fungu lake la Rozari. Mungu hufurahishwa sana na wenye kusali Rozari Hai, na hivyo huwajaza mema mengi sana. Kila mwanachama anaposali kumi lake, humwomba Mungu Neema za pekee kwa ajili yake mwenyewe, na pia kwa ajili ya wanachama wenzake, na hasa kwa kuwaombea wakosefu waongoke. Neema tuombazo ni zile walizostahili Yesu na Mama yake katika fumbo tunalotafakari.
Kwa wale walioamua kusali Rozari nzima kila siku yaani tasbihi tatu: mafumbo ya furaha ya Uchungu na ya utukufu, hao hawana tena lazima ya kusali kumi jingine kwa kutimiza Rozari yao Hai. Wanachotakiwa kufanya ni kuweka tu nia wanaposali kumi lao. Lakini hakatazwi kuongeza kumi nyingine, ni hiari yake.
Kumi lako Rozari Hai unaweza kulisali wakati wowote na katika nafasi yeyote ile: mchana, usiku, na popote pale, hata unapofanya kazi.